Wilaya inazo shule 20 za Sekondari zenye jumla ya wanafunzi 3,403 kati yao wasichana ni 1,637 na wavulana ni 1,766. Idadi ya walimu waliopo ni 356 (wanaume 237 na wanawake 119) kati ya mahitaji ya walimu 394. Hivyo Wilaya ina upungufu wa walimu 38. Walimu wa sayansi waliopo ni 70, mahitaji ni walimu 160, upungufu ni walimu 90.
Aidha, jumla ya wanafunzi 1,651 (wav. 753, was. 898) walifaulu darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwezi Januari 2017.
Katika kuboresha miundombinu mashuleni kwa kipindi cha 2015/2016 jumla ya nyumba 3 (1kwa 6) vyoo 8 na vyumba 4 vya madarasa vimejengwa, katika shule za Msisi, Chonama na Magaga. Nyumba za walimu katika shule za Msisi na Magaga zimekamilika na Chonama ujenzi unaendelea. Pamoja na shule hizo hadi sasa wilaya inazo shule 4 zenye maabara ambazo ni Chikola, Chibelela, Mundemu na Bahi.
Ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari uko katika hatua mbalimbali ambapo maabara 5 zimekamilika, 14 hatua ya umaliziaji, 11 hatua ya upauaji, 2 zipo katika hatua ya lenta, 6 hatua ya ukuta, 10 hatua ya msingi, na 12 bado hazijaanza.
Aidha, Wilaya imeanzisha klabu za wasichana katika shule zote 20 (ishirini) za Sekondari ambazo zimesaidia kupunguza utoro mashuleni na mimba.
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 755 352 875
Simu: +255 689 571 881
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa