HISTORIA:
SURA YA WILAYA
Wilaya ya Bahi ni mojawapo kati ya Wilaya saba za Mkoa wa Dodoma. Wilaya hii ilianzishwa rasmi mwaka 2007 na ina jumla ya kilometa za mraba 5,948 ikiwa na Tarafa 4, Kata 22, Vijiji 59 na vitongoji 553. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ina watu 221,645 kati yao wanaume ni 105,975 (47.8%) na wanawake ni 115,670 (52.2 %).
UCHUMI WA WILAYA
Uchumi wa Wilaya unatokana na shughuli za kilimo na ufugaji. Mazao ya chakula ni mtama, uwele, viazi vitamu, mihogo, mahindi, mpunga, kunde, mbaazi, na njugu. Mazao ya biashara ni pamoja na ufuta, alizeti na karanga. Aidha, mifugo inayofugwa ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, kuku, bata na kanga.
Makadirio ya pato la mkazi kwa mwaka 2007 yalikuwa 206,000.00, kwa sasa inakadiriwa pato hili kuongezeka hadi kufikia 427,489 sawa na 207.5% ya ongezeko.
HALI YA KISIASA
Hali ya kisiasa ni shwari ambapo Wilaya ina vyama saba vya siasa vinavyofanyakazi ambavyo ni CCM, CUF, SAU, CHADEMA, TLP, NCCR- Mageuzi na ACT –Wazalendo. Aidha, Wilaya ina Madiwani 22 wa kuchaguliwa, 6 viti maalum na Mbunge 1 wa kuchaguliwa; Hali ya ulinzi na usalama ni nzuri na vyombo vyote vya dola kwa pamoja vinatimiza wajibu wake.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa