Benton Nollo na Bernard Magawa, Bahi
Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021, Luteni Josephine Mwambashi amezindua mradi wa matumizi ya TEHAMA kwenye huduma za maji safi kupitia mradi mpya wa kutumia malipo ya kabla (Pre Paid) katika Kijiji cha Zanka tarehe 25 Julai 2021.
Mradi huo unaolenga kupunguza upotevu wa maji yaliyokuwa yakipotea bila kulipiwa na kupunguza gharama za uendeshaji, umezinduliwa rasmi na kiongozi huyo baada ya kujiridhisha na utekelezaji wake.
Akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda amemshukuru Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 kwa kuuzindua mradi huo ambao amesema utawapunguzia kero akinamama ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Awali, akisoma taarifa ya mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021, Mratibu wa Mradi Mhandisi Robert Mgombela amesema mradi huo umegharimu shilingi milioni 181 hadi kukamilika kwake ambao umetekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Benki ya Dunia kupitia Benki ya TIB na Wataalamu washauri wa Shirika Lisilo la Kiserikali liitwalo OIKOS East Africa.
“Tumekarabati vituo 11 vya kuchotea maji kwa kuweka mita za malipo ya kabla (pre-paid meter) na kufunga mashine za mfumo katika vituo vyote na tayari wananchi wameanza kununua maji kupitia kadi maalumu za kielektroniki (token) ambazo mtumiaji huingiza fedha kwa kutumia simu ya mkononi kupitia Mpesa, Tigopesa, Airtel Money na Halopesa (kwa wale wenye simu) au kupitia kwa wakala kwa wale ambao hawana simu za mkononi.” Amesema Mgombela.
Matukio katika Picha:
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 687748878
Simu: +255 687748878
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa