Leo Tarehe 6/11/2025 Halmashauri kupitia kitengo Cha Lishe katika kimefanyika kikao kijadili Hali ya Lishe katika Halmashauri ya Bahi.
Kupitia kikao hicho kilichofanyika katika ofisi Mkurugenzi mtendaji Bi.Albina w.Mtumbuka kitengo cha Lishe kiliwasilisha taarifa inayotoka tathimini ya Lishe katika Wilaya hiyo nakuoneaha jinsi ambavyo kitengo cha Lishe
Kimefanikiwa kutoa elimu ya Lishe kwa wamama 30,048 wenye watoto chini ya miaka 5., imefanikiwa kufanya upimaji kwa watoto 28,507 wa chini ya miaka 5 ambapo watoto 20 walikuwa wamedumaa,watoto 92 wana ukondefu na watoto 22 wanao utapiamlo mkali ambao wote kwa pamoja wapo kwenye matibabu.
Pia,taarifa hiyo ya Lishe imeonesha Wajawazito wanaaswa kuhudhuria kliniki na kuendelea kutumia vidonge vya madini ya chuma(FEFO) ili kujikinga na upungufu wa damu.
Wamama wanaonyonyesha wameaswa kuhakikisha wananyonyesha watoto wao kwa miezi 6 ya mwanzo bila kuwachanganyia na kitu chochote kupunguza athari za udumavu na ukondefu.
Aidha ,Halmashauri inaendelea kuhamasisha wenye mashine za kusaga unga kuweza kufunga mashine zenye kurutubisha unga ili Wananchi waweze kutumia unga wenye kurutubishwa ambao unanyongeza ya vitamin na madini.
Mtaalam wa Lishe wa Wilaya Bi.Gloria Ngowi amesema Jamii inapaswa kuendelea kufuata misingi ya ulaji unaofaa kupunguza athari za magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
Anuani: S.L.P 2993 DODOMA
Simu: +255 762077589
Simu: +255 762077589
Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa