• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
BAHI DISTRICT COUNCIL
BAHI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kazi na Moto
      • Afya
      • Maji
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Tehama na Uhusiano
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mpiango
      • Ujenzi,Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokubaliwa
    • Miradi Inayoendelea
      • TASAF
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Kazi
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbali Mbali
    • Miongozo Mbali Mbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video Mbali Mbali
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kipanga: Ujenzi Vyuo vya VETA Nchini Mwisho Machi 2021

Imechapishwa: January 20th, 2021

Na Benton Nollo na Bernard Magawa (DMC), Bahi

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (Mb) ameagiza ujenzi wa vyuo vyote vya VETA unaoendelea nchi nzima kukamilika kabla ya tarehe 31 Machi 2021 ili majengo hayo yaanze kutumika mwaka huu.

Kipanga ametoa agizo hilo tarehe 20 Januari 2021 alipotembelea na kukagua ujenzi wa chuo cha VETA Wilaya ya Bahi ambapo hakuridhishwa na kasi ya ujenzi wa chuo hicho ambao unasimamiwa na Uongozi wa Chuo hicho kwa kutumia Force Account kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6.

“Binafsi niseme wazi sijaridhishwa kabisa na mwenendo wa ujenzi wa chuo hiki na namna mlivyoandaa mpangilio wa kazi zenu, nitarudi tena hapa baada ya wiki moja na nitakapo kuja nikute kila jengo lina fundi wake na wanafanya kazi vinginevyo tusilaumiane kwani siwezi kuacha uzembe huu uendelee.” Amesema Kipanga na kuongeza;

“Niagize wale wote wanaosimamia miradi ya ujenzi wa vyuo vya VETA nchini kuhakikisha wanakamilisha miradi hii kabla ya tarehe 31 Machi 2021, na viongozi wa maeneo hayo simamieni kikamilifu ujenzi huo ili majengo hayo yaweze kufunguliwa na kuanza kazi mapema mwaka huu.”

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri huyo, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda ameahidi kusimamia kwa ukaribu na kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka iwezekanavyo.

“Ujenzi umekuwa wa kusuasua sana, hata mimi sifurahishwi wala siridhishwi na ujenzi wa chuo chetu cha VETA Bahi, tuna watoto wengi mitaani ambao hawakufaulu kuendelea na masomo mengine na hatuna pa kuwapeleka zaidi ya VETA, sielewi tatizo liko wapi labda kwa sababu mamlaka haipo Halmashauri ipo wizarani.” Amesema Munkunda na kuongeza;

“Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kweli hili linatuchafua sisi kama Wilaya kwa sababu mambo haya hatujazoea, sisi tumekuwa tukifanya vizuri katika miradi mingine ambayo fedha zilipita Halmashauri.”

Naye, Makamu Mkuu wa Chuo cha VETA Mkoa wa Dodoma, Stanslaus Ntibala amesema kusuasua kwa ujenzi huo kunatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo vifaa vya ujenzi kuchelewa kupelekwa na wazabuni ilhali tayari walishalipwa.

 Ujenzi wa chuo cha VETA Bahi unaojumuisha ujenzi wa majengo 17 ulianza mwezi Mei 2020 na ulitakiwa kukamilika mwezi Desemba 2020.

Matangazo

  • Tangazo la Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani Kujadili Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 February 10, 2021
  • Tangazo la Kikao cha Baraza la Madiwani January 27, 2021
  • Tangazo la Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2021 Wilaya ya Bahi December 18, 2020
  • Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili Nafasi za Kazi za Mtendaji wa Kijiji Daraja la III November 02, 2020
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mabati 780 Yanunuliwa, Mfuko wa Jimbo

    February 12, 2021
  • Baraza la Madiwani Lapitisha Bajeti ya Shilingi Bilioni 25

    February 12, 2021
  • Watakaonunua Ardhi, Wenye Leseni za Madini Ujenzi Kuchangia Elimu

    January 29, 2021
  • Mfuko wa Jimbo Kusaidia Ujenzi wa Madarasa, Zahanati

    January 28, 2021
  • Tazama Zote

Video

RC MAHENGE AZITAKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DODOMA KUAINISHA FURSA ZA UWEKEZAJI.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Tazama na Kudownload Orodha ya Walioitwa Kwenye Interview kwa Nafasi za Watendaji wa Vijiji Bahi
  • Matokeo Kidato cha Nne 2017
  • Tazama matokeo ya Darasa la saba 2019 ya shule zote za Bahi
  • Tazama na Kudownload vigezo vya Nafasi za Kazi kwa Watendaji wa Vijiji
  • Matokeo ya QT
  • 1: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Darasa la Nne (SFNA) 2017
  • Vendor Form
  • 2: Matokeo ya Upimaji wa Kitaifa Kidato cha Pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • OR-TAMISEMI
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Dodoma
  • Tovuti ya Ikulu

Watembeleaji wa Nje

world map hits counter

Watembeleaji

Counter Widgets

Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

    Anuani: S.L.P 2993 DODOMA

    Simu: +255 26 2961400

    Simu: +255 766 643 266

    Barua Pepe: ded@bahidc.go.tz

Mawasiliano Zaidi

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Haki Zote Zimehifadhiwa